Friday, February 8, 2013

KAFIRI NI NANI?

Swali:
Naitwa mwinjilisti Onesmo, Kwanini nyie waislamu mnatuita sisi wakristo makafiri?

Jibu:
Nashkuru kwa swali lako.

Hatuwaiti hivyo kwa utashi wetu bali ni MwenyeziMungu (Allah) mwenyewe ndo kasema katika kitabu kitakatifu cha Quran 5:72-73

QURAN 5:72-73
72. Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! 
Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.
TAFSIRI:

Wenye kudai kuwa Mwenyezi Mungu yu katika Isa bin Maryam hata akawa yeye Mungu, kama wasemavyo Wakristo hii leo, hakika wamekufuru! Yeye Isa hana dhambi ya haya, kwani hakupata kudai hivyo hata mara moja. Bali yeye aliwaamrisha Wana wa Israili wamsafie imani Mwenyezi Mungu peke yake kwa kusema: Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye niumba mimi na nyinyi, na ndiye anaye niendeshea mambo yangu yote, na kwamba kila mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu malipo yake ni kuwa hatoingia Peponi kabisa, bali ataingia Motoni, kwa kuwa amekiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kuvunja mipaka yake hataepuka na adhabu.(Yesu kasema: "Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja." Marko 12.28. "Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe".Yohana 5.30 "Ninapaa kwenda kwa...Mungu wangu naye ni Mungu wenu." Yohana 20.17 ) 

73. Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja. 
Na ikiwa hawaachi hayo wanayo yasema, kwa yakini itawakamata adhabu chungu wale wanao kufuru
 TAFSIRI:
Haiwi mwenye kudai kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja katika Utatu, kama wadaivyo Wakristo sasa, awe anamuamini Mwenyezi Mungu.!! Na hakika iliyo thibiti ni kuwa hapana mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja pekee. Na ikiwa hawa walio potoka hawatoacha itikadi zao potovu, wakarejea kwenye ut'iifu wa Mwenyezi Mungu, hapana budi ila itawasibu adhabu kali. (Biblia inasema kuwa ya kwanza katika Amri Kumi alizo pewa Musa ni: "Usiwe na miungu mingine ila mimi." - Kutoka 20.3. "Wewe umeonyeshwa haya, ili upate kujua ya kuwa Bwana ndiye Mungu, hapana ila yeye." - Kumbukumbu la Torati 4.35. Katika Injili ya Yohana 17.3 Yesu anamsemeza Mwenyezi Mungu: "Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.") 


Kwahiyo tunawaita makafiri kwa sababu miongoni mwenu mnamwita Yesu kuwa ni Mungu na miongoni mwenu mnasema kuwa Mungu ni wa tatu wa utatu.

No comments:

Post a Comment

Animated Social Gadget - Blogger And Wordpress Tips Twitter Bird Gadget