Thursday, April 26, 2012

Kwanini waislamu mnasema Yesu si Mwana wa Mungu?

Jibu:
Huenda hufahamu maana halisi ya neno Mwana wa Mungu.
Tuangalie ushahidi uliopo katika Biblia, huenda ukaelewa uhalisia wa neno Mwana wa Mungu.
Biblia inasema kwamba:
1. Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu.(Kutoka 4:22).

2. Daudi ni mwana wa Mungu, yeye pia ni mwana wa kwanza. (Zaburi 89: 26-27).

3. . . . .maana mimi ni baba wa Israel i na Ef raim (Ibrahim) ni mzaliwa wa kwanza wangu. (Yeremia31:9). Hawa wana wa Mungu wote, kila mmoja wao ni mzaliwa wa kwanza kwa Mungu.

Kwanza itakuwaje watoto wote watatu wawe wazaliwa wa kwanza kwa Mungu?

Pili kwa nini hawa wazaliwa wa kwanza wasiitwe miungu?

Na kama hawa watatu wakubwa hawawezi kuwa miungu wala hawaabudiwi, basi mtoto mdogo Yesu pia hana haki yoyote ya kuitwa Mungu wala hana haki ya kuabudiwa.

OKEY TUENDELEE:
4. Suleimani ni Mwana wa Mungu. (Mambo ya Nyakati 22:9-10).

5. Wa p a t a n i s h a o w a m e i t w a Wa n a w a M u n g u.(Mathayo 5:9).

Oo! siyo tu bali katika Biblia baadhi ya watu wameitwa miungu. Tena hakuna Mkristo ambaye anawaita miungu wala hawaabudiwi. 

Kama Biblia inavyosema kwamba:
A. Yesu akawajibu, Je! haikuandikwa katika Torati yenu ya kwamba, mimi nimesema, ndinyi miungu? (Yohana 10:34).
B. Bwana akamwambia Musa angalia, nimekufanya wewe kuwa kama mungu kwa Farao na huyo ndugu yako Harun atakuwa Nabii wako. (Kutoka 7:1)
Hivyo basi;
Mwana wa Mungu maana yake ni kipenzi cha Mungu, yaani anayefata na kutekeleza maagizo ya Mwenyezi Mungu.

No comments:

Post a Comment

Animated Social Gadget - Blogger And Wordpress Tips Twitter Bird Gadget