Wednesday, April 25, 2012

Yesu atawezaje kuhukumu kutumia Qur'an ambayo ina mafundisho mengi yanayopingana na mafundisho yake?

Ni kweli kuwa Yesu (A.S) atarudi na kubainisha haki na batili..

Ushahidi ni huu hapa:


Volume 4, Book 55, Number 657 :
Narrated by Abu Huraira
Allah's Apostle said, "By Him in Whose Hands my soul is, surely (Jesus,) the son of Mary will soon descend amongst you and will judge mankind justly (as a Just Ruler); he will break the Cross and kill the pigs and there will be no Jizya (i.e. taxation taken from non Muslims). Money will be in abundance so that nobody will accept it, and a single prostration to Allah (in prayer) will be better than the whole world and whatever is in it." Abu Huraira added "If you wish, you can recite (this verse of the Holy Book): 'And there is none Of the people of the Scriptures (Jews and Christians) But must believe in him (i.e Jesus as an Apostle of Allah and a human being) Before his death. And on the Day of Judgment He will be a witness Against them." (4.159) (See Fateh Al Bari, Page 302 Vol 7)

Volume 4, Book 55, Number 658 :Narrated by Abu Huraira
Allah's Apostle said "How will you be when the son of Mary (i.e. Jesus) descends amongst you and he will judge people by the Law of the Quran and not by the law of Gospel (Fateh-ul Bari page 304 and 305 Vol 7)
Sasa hebu turudi katika maandiko:

Katika Matayo 7:3-5,Yesu anasema hivi:
7:3 Kwa nini wakiona kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako?
7:4 Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, `Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako`, wakati wewe mwenyewe unayo boriti jichoni mwako?
7:5 
Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako na hapo ndipo utaona waziwazi kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichoko jichoni mwa ndugu yako.
Hapo Yesu (Amani ya Bwana iwe naye) anamaanisha kwanza kuwa tujirekebishe kwanza kabla ya kukosoa wenzetu.

Sasa, ingekuwa busara uangalie kwanza makosa yaliyopo katika Biblia (unayoiamini) kabla ya kuonesha udhaifu wa Qur'an ambayo huiamini.

Huenda unajua au hujui, hizi hapa ni baadhi ya contradictions zilizopo kwenye Bible;

Ntakupa mifano mitatu tuu kuwakilisha.

Mfano wa kwanza;
2 wafalme 8:26

Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala...

2 Nyakati 22:2

Ahazia alikuwa na umri wa miaka arobaini na miwili alipoanza kutawala...

Sasa hapo sahihi ni ipi?


Mfano wa pili:
2 Samweli 24:1
Tena hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli
akamtia Daudi nia juu yao, akasema, Nenda ukawahesabu Israeli na Yuda.

1 Nyakati 21:1
Tena Shetani akasimama juu ya Israeli, akamshawishi Daudi,kuwahesabu Israeli.

Sasa hapo sahihi ni ipi?


Mfano wa Tatu:
2 Samweli 10:18

Wakakimbia Washami mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari mia saba, na wapanda farasi arobaini elfu, naye akampiga huyo Shobaki, jemadari wa jeshi lao, hata akafa huko.

1 Nyakati 19:18
Washami wakakimbia mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari saba elfu, na askari waendao kwa miguu arobaini elfu na akamwua na Shobaki, jemadari wa jeshi. 

Sasa hapo sahihi ni ipi?

No comments:

Post a Comment

Animated Social Gadget - Blogger And Wordpress Tips Twitter Bird Gadget