Swali:
Je hamjui kuwa Yesu ni Mungu na ndo maana ana uwezo wa kufufua wafu? Mwenyewe anasema "Nami ninao uwezo wa kuutoa, ninao na uwezo wa kuutwaa tena..(Yoh 10:18)"
Jibu:
Unashangaa Yesu kufufua/kuhuisha wafu?
Ikiwa kwa sababu ya kufufua wafu hawaitwi miungu, basi Yesu pia hana haki yoyote ya kuitwa Mungu. Biblia inasema:
1. Elisha alifufua mtoto aliyefariki. (2 Wafalme 4:35).
2. Maiti alifufuka kwa kuguswa na mifupa ya Elisha. (2 Wafalme 13:3:21).3. Ezekiel alifufua jeshi kubwa. (Ezekiel 37:10)
Halafu, mbona hujamalizia andiko?
Andiko liko hivi:
Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.
Kiingereza:
No man taketh it from me, but I lay it down of myself. I have power to lay it down, and I have power to take it again.This commandment have I received of my Father.
Kwa maana hiyo, Yesu anaweza kujitoa uhai na kujirudishia kwa uwezo alopewa na Baba(Mungu)
Lakini hichi sio cha kushangaza maana hata Mfalme Daudi/King David alipewa uwezo wa kudhibiti na kuamrisha viumbe kuanzia wadudu, majini mpaka upepo.
No comments:
Post a Comment