Saturday, May 5, 2012

Je mwaweza nipa maandiko ya Biblia yanayokataza ulevi?

Swali:
Mimi ni mnywaji  mzuri wa divai (pombe), lakini kuna rafiki yangu  mwislamu kanihubiria kuwa ulevi umekatazwa hadi katika Biblia, Je mwaweza nipa maandiko ya Biblia yanayokataza ulevi?


Jibu:
Yafuatayo ni baadhi ya maandiko yanayo dhihirisha uharamu wa ulevi.


Uzinzi na divai, na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.(Hosea 4:11)


Ole wa taji ya kiburi ya walevi wa Efraim na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalostawi la hao walioshindwa na divai! (Isaya 28:1).

Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu huchanganya vileo, wampao haki mwenye uovu ili wapewe ijara na kumwondolea mwenye haki haki yake. (Isaya 5;22-23).

Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo, wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao! Na kinubi, na zeze na matari na filimbi, na mvinyo zote ziko katika karamu zao lakini hawaangalii kazi ya Bwana wala kuyafikiri matendo ya mikono yake. (Isaya 5:11-12

Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu, litiapo bilauri rangi yake ishukapo taratibu; mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira. Macho yako yatakuwa mambo mageni; na moyo wako utatoa yaliyopotoka,Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti. 

Utasema,wamenichapa wala sikuumia, wamenipiga wala sina habari, Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.(Mithali 23:31-35).

Wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia, huota ndoto, hulala, hupenda usingizi. Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno, wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe kila mmoja kwa faida yake toka pande zote. Husema, njooni nitaleta divai,na tunywe sana kileo na kesho itakuwa lama leo sikukuu kupita kiasi.(Isaya 56:10-12).

No comments:

Post a Comment

Animated Social Gadget - Blogger And Wordpress Tips Twitter Bird Gadget