Tuesday, May 1, 2012
What happened to the previous scriptures?
Question:
What happened to the previous scriptures?
Answer:I start in the name of Allah.Here in below are answers:
(4:46); Among those who are jews, there are some who displace words from (their) right places and say: “We hear your word (O Muhammad (PBUH)) and disobey,” and “Hear and let you (O Muhammad (PBUH))
Translation:“hear nothing.” And Raina with a twist of there tongues and as a mockery of the religion (Islam) And if only they had said: “We hear and obey”, And “Do make us understand,” it would have been better for them, and more proper; but Allah has cursed them for their disbelief, so they believe not except a few.
Kiswahili:
4:46. Miongoni mwa Mayahudi wamo ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahala pake, na husema: Tumesikia na tumeasi, na sikia bila ya kusikilizwa. Na husema: "Raai'naa", kwa kuzipotoa ndimi zao ili kuitukana Dini. Na lau kama wangeli sema: Tumesikia na tumet'ii, na usikie na "Undhurna" (Utuangalie), ingeli kuwa ni kheri kwao na sawa zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru yao; basi hawaamini ila wachache tu.
Tafsiri:
Miongoni mwa Mayahudi kipo kikundi kazi yao kugeuza geuza maana ya maneno. Wao husema kimoyomoyo kumwambia Mtume s.a.w.: Tumesikia hayo maneno, na hatuifati hiyo amri. Na pia husema: Sikia maneno yetu - hukusikia wito. Wakikusudia kwa hayo kumuapiza Mtume. Na husema: Sikia bila ya kusikilizwa. Tamko hilo wanalipindua maana. Muradi wao ni kumuapiza, na wanajidai kuwa muradi wao ni kumwombea dua. Na husema: "Raai'na", wakipindua ndimi zao wakijitia kuwa wanakusudia "Undhurna" yaani "Tuangalie". Wanaonyesha kuwa wanataka uangalizi wake, na kumbe wanakusudia neno la Kiyahudi lenye maana ya "Mpumbavu" ili kuibeza Dini ya Kiislamu.
Na lau kuwa wangeli nyooka sawa wakasema: "Tumesikia na tumet'ii" badala ya hiyo kauli yao ya "Tumesikia na tumeasi", na wakasema: "Sikia" na wasiseme "Bila ya kusikilizwa", na wakasema :"Undhurna" yaani "Tuangalie", badala ya "Raa'ina", ingeli kuwa bora kwao kuliko hayo wayasemayo, na ingeli kuwa ndiyo njia ya uadilifu zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu amewatoa katika rehema yake kwa ule upinzani wao. Kwa hivyo huwaoni miongoni mwao wanao mwitikia mwenye kuwaitia Imani ila wachache tu.
(5:13) So because of their breach of their covenant, We cursed them and made their hearts grow hard. They change the words from their (right) places and have abandoned a good part of the Message that was sent to them. And you will not cease to discover deceit in them, except a few of them. But forgive them and overlook (their misdeeds).Verily, Allah loves Al-Muhsinun (good-doers).
Kiswahili:5:13:
Basi kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani, na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyo kumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipo kuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na waache. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema
Tafsiri:Basi kwa sababu ya Wana wa Israili kuvunja agano lao ndio wakastahiki kufukuzwa kutokana na rehema ya Mwenyezi Mungu. Nyoyo zao zikawa ngumu, si laini za kupokea Haki; na wakaingia kupotoa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyomo katika Taurati kutokana na maana yake ya asli, na yafuate yanayo wafikiana na wapendavyo wao. Wakaachilia mbali pande kubwa ya mambo waliyo amrishwa katika Taurati !! Na wewe, Mtume, huachi kuona kila namna ya khadaa na uvunjaji wa ahadi kwa hawa Wana wa Israili, isipo kuwa kwa wachache tu miongoni mwao ambao wanakuamini wewe. Hao hawakhuni wala hawadanganyi. Basi, ewe Mtume! Yasamehe yaliyo pita kutokana na watu hawa, na wachilia mbali, bali wafanyie wema. Kwani Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment