Friday, May 4, 2012

Mungu anasifa gani ambazo Yesu hana?

Swali:
Nyie waislamu mnapenda kukanusha kuwa Yesu sio Mungu, kwani kwa upeo wenu mnadhani ili Yesu awe Mungu anastahili kuwa na sifa gani?


Jibu:
Ni kweli kuwa Yesu ni mtume tuu na wala hana sifa ya kuwa Mungu.
Tutumie maandiko yaliyo katika Biblia mnayoiamini katika kutofautisha kati ya Mungu na Yesu.


Yakobo 1:13). Mungu hajaribiwi na Shetani.
 (Mat 4:1). Lakini Yesu alijaribiwa na Iblisi.
(Isaya 40:28).Mungu hachoki.

(Yoh. 4:6)Lakini Yesu alichoka


(Ezekiel 28:8-9).Mungu hauwawi

(Matendo 5:30)Lakini Yesu aliuwawa


Mungu hafi (Daniel 6:26).
Lakini Yesu alikufa (Mat. 27:50)


(1Wafalme 8:39)Mungu anajua kila kitu.
Lakini Yesu hakujua kila kitu (mti wa mtini).(Mat. 21:18-19) 
Ilhali haukuwa msimu wa matunda (Marko 11:13)




Mungu hali, lakini Yesu aliona njaa na akala.(Marko 11:12; Luka 11:37-38, 24:42-43)

(Zaburi 121:3-4).Mungu hasinzii. 
Lakini Yesu alilala fofofo.(Marko 4:37-38; Mat. 8:23-25)

No comments:

Post a Comment

Animated Social Gadget - Blogger And Wordpress Tips Twitter Bird Gadget