Kwanini waislamu mnasema maandiko ya biblia yanahitilafu?
Jibu:
Yafuatayo ni mahitlifiano ya maandiko katika biblia.
Michael
binti wa Saul hakupata mtoto mpaka kifo chake.(2 samweli 6:23)
Michael
binti wa Saul alikuwa na wavulana watano (2 Samweli 21:8)
Benjamin
alikuwa na watoto watatu. (1 Mambo ya Nyakati 7:6)
Benjamin
alikuwa na watoto watano. (1 Mambo ya Nyakati 8:1-2.
Harun
alikufa huko Hor. (Hesabu 33:38)
Haruni
alikufa huko Mosera (Kumb. 10:6)
Yehoremu
alishikilia kutawala wakati akiwa na umri wa mika 32 alifariki katika miaka 40,(2
Mambo ya Nyakati 21:5) (2 Mambo ya Nyakati 21:20).
Baada ya
kifo chake mtoto wake mdogo alishikilia serikali na alikuwa na umri wa miaka 42
wakati ule.(2 Mambo ya Nyakati (22:1-2).
Kana
kwamba mwana mdogo alikuwa miaka miwili zaidi kuliko baba mzazi! (9. Mat 5:17;
Mat 5:38-40; Hebrew 7:12).
Sungura
hucheua (Mambo ya Walawi 11:6). Lakini ukweli ni kwamba Sungura hacheui kabisa.
Yuda
aliyemsaliti Yesu alivitupa vile vipande vya fedha alivyopewa kwa udhalimu wake
huo, kisha alijinyonga na
wakuu wa
Makuhani wakavichukua vipande vya fedha na wakanunulia shamba la kuzikiwa watu
(Mat 27:5-7).
Lakini
(Matendo 1:18), inasema kwamba Yuda mwenyewe alinunua konde kwa ijara
aliyoipata kwa udhalimu wake huo na kisha akaanguka na kupasuka na matumbo yake
yote yakatoka.
Yesu
alifyolewa na wanyang’anyi wawili aliposulubiwa pamoja nao. (Marko 15:32 ; Mat.
27:44).
Lakini
katika Luka 23:39-40, inasema kuwa mnyang’anyi mmoja ndiye aliyemfyolea Yesu.
Yuda
alijinyonga.(Mat. 27:5).
Lakini katika
Matendo 1:18, imeandikwa kwamba alianguka na kupasuka matumbo yake
Mwanadamu
aliumbwa baada ya uumbaji wa wanyama.(Mwanzo 1:25-26).
Lakini
katika (Mwanzo 2:18-20), inaonekana mwanadamu aliumbwa kwanza.
Mwandishi
wa Torati siye Nabii Musa mwenyewe.
Basi Musa
mtumishi wa bwana akafa huko katika nchi ya Moabu kwa neno la Bwana. (Kumb.
34:5).
Mwandishi
wa Kitabu cha Mathayo si Mathayo mwenyewe ambaye ni mwanafunzi wa Yesu.(Mat.
9:9).
No comments:
Post a Comment