Tuesday, May 8, 2012

Nini maana ya Kristo?

Swali:
Mimi ni mpagani na ningependa kujua maana halisi ya neno "kristo"


Jibu:
Neno KRISTO linatokana na neno Messiah la Kiebrania. 
Kwa Kiarabu ni Masih. 
Shina la neno ni m-a-s-a-h-a, maana yake ni kuchuwa, kusinga, kupaka. 
Makuhani na wafalme walisingwa (walipakwa mafuta) kabla ya kusimikwa katika katika nyadhifa zao. Lakini kwa haiba yake ya tafsiri ya Kigiriki, neno hili linaonekana kuwa mahususi, likiswihi kwa Yesu tu.
Mkristo ana mazoweya ya kubadilisha metali kuwa dhahabu ing’arayo. Walichoweza kukifanya ni kuyabadili kabisa maneno katika lugha yake kama vile “Cephus” kuwa Peter, “Messiah” kuwa Christ.
Anawezaje kufanya hivyo? Rahisi sana. Neno MASSIAH la Kiebrania, kwa Kiingereza, maana yake ni Anointed (aliyepakwa, aliyetiwa au aliyesingwa mafuta). Neno la Kigiriki la kutafsiri neno hilo ni “christos”. 
Inyofowe ‘os’ katika neno christos, hapo unabakiwa na christ. Sasa geuza “c” ndogo kuwa “C” kubwa, yebo! Hapo sasa keshaunda jina jingine!
Christos maana yake ni ALIYETIWA (ALIYEPAKWA) MAFUTA, na mpakwa mafuta, kwa maana yake ya kidini ni MTEULE (ALIYETEULIWA). Yesu (as), baada ya ubatizo wake kwa Yohana, aliteuliwa kuwa nabii wa Mungu. Kila nabii wa Mungu huteuliwa hivyo (anointed or appointed).
Biblia imejaa “wapakwa mafuta” kibao. Yaani kwa lugha asiliya ya Kiebrania-waliofanywa kuwa “messiah”. Hebu tubakiye na tafsiri hiyo ya Kiingereza- “anointed.” 
Siyo tu manabii makuhani na wafalme waliotiwa mafuta (christos-ed- waliofanywa kristo) bali pembe, kerubi na nguzo nazo piya zilitiwa mafuta (zilifanywa kristo)
Kama Kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi... (mambo ya walawi 4:3)
Kisha Musa akatwaa hayo mafuta matakatifu ya kutia, akatia mafuta maskani, na vyote vilivyokuwamo, na kuvitakasa...(mambo ya walawi 8:10)
Bwana.... Na kuitukuza pembe ya masihi wake (1Samweli 2:10)
Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake...(Isaya 45:1)
Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta.... (Ezekieli 28:14)


Kuna zaidi ya mifano mia kama hiyo katika Biblia. Kila ukutanapo na neno anointed katika lugha ya Kiingereza (iliyotumika kutafsiri Biblia kwa Kiswahili), uchukuliye kuwa neno hilo ni christos kwa tafsiri ya Kigiriki.

Na ukilichukuwa neno christ ambalo wakristo wameliunda, utakuwa na Christ Cherub (Kerubi Kristo), Christ Cyrus (Koreshi Kristo), Christ Priest (Kuhani Kristo), Christ Pillar (Nguzo Kristo) n.k.

9 comments:

Animated Social Gadget - Blogger And Wordpress Tips Twitter Bird Gadget